Al-Qasas 28:37
القصصوَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّىٓ أَعْلَمُ بِمَن جَآءَ بِٱلْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِۦ وَمَن تَكُونُ لَهُۥ عَـٰقِبَةُ ٱلدَّارِ ۖ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Na Musa akasema, "Mola wangu Mlezi ni Mwenye kujua kabisa ni nani anayekuja na uongofu unaotoka kwake, na ni nani atakayekuwa na mwisho mwema wa makazi. Hakika wenye kudhulumu hawatafanikiwa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Musa akasema: Mola wangu Mlezi ni Mwenye kujua kabisa nani anaye kuja na uwongofu unao toka kwake, na nani atakaye kuwa na mwisho mwema wa makaazi. Hakika wenye kudhulumu hawatafanikiwa. [37]
[37] Na Musa alisema kumjibu Firauni na kaumu yake: Mola wangu Mlezi anajua kwa hakika kuwa mimi nimeleta Ishara hizi zenye kuonyesha Haki na Uwongofu kutokana naye Yeye. Basi Yeye ndiye shahidi wangu kwa haya, ikiwa nyinyi mnanikadhibisha. Na Yeye anajua kuwa mwisho mwema ni wetu sisi watu wa Haki. Hakika makafiri hawapati kheri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Mûsã alisema kumwambia Firáwn, «Mola wangu Anamjua zaidi aliye kwenye sawa kati yetu, aliyekuja na uongofu kutoka Kwake, na yule atakayekuwa na mwisho wa kushukuriwa katika Nyumba ya Akhera. Kwa hakika, madhalimu hawatayapata matakwa yao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net