Al-Qasas 28:36
القصصفَلَمَّا جَآءَهُم مُّوسَىٰ بِـَٔايَـٰتِنَا بَيِّنَـٰتٍ قَالُوا۟ مَا هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِىٓ ءَابَآئِنَا ٱلْأَوَّلِينَ
Basi Musa alipowafikia na Ishara zetu, walisema, "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi uliozuliwa. Na hatukuyasikia haya kwa baba zetu wa zamani."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi alipo wafikia Musa na Ishara zetu, walisema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio zuliwa. Na hatukuyasikia haya kwa baba zetu wa zamani. [36]
[36] Musa alipo wakabili kwa wito wake ulio tiliwa nguvu na miujiza iliyo wazi, waliyakanusha waliyo yaona, na wakasema: Haya si chochote ila ni uchawi unao mzulia Mwenyezi Mungu. Na hatukupata kusikia haya unayo tuitia kwa baba zetu wa zamani walio tangulia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mûsã alipomjia Firáwn na viongozi wa mamlaka yake na aya zetu na hoja zetu zenye kushuhudilia ukweli wa yale aliyokuja nayo kutoka kwa Mola wake, walimwambia Mûsã, «Hili ulilotujia nalo si chochote isipokuwa ni uchawi uliouzua kwa urongo na ubatilifu. Na hatujawahi kusikia jambo hili unalotuitia kwalo kutoka kwa wale waliotutangulia waliopita kabla yetu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net