Al-Qasas 28:35
القصصقَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَـٰنًا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيْكُمَا ۚ بِـَٔايَـٰتِنَآ أَنتُمَا وَمَنِ ٱتَّبَعَكُمَا ٱلْغَـٰلِبُونَ
(Mwenyezi Mungu) akasema, "Tutautia nguvu mkono wako kwa kaka yako, na tutawapa mamlaka, kwa hivyo hawatawafikilia. Kwa sababu ya Ishara zetu, nyinyi na watakaowafuata ndio mtashinda."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
(Mwenyezi Mungu) akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa nduguyo, na tutakupeni madaraka, hata wasikufikilieni. Kwa sababu ya Ishara zetu nyinyi na watakao kufuateni mtashinda. [35]
[35] Mwenyezi Mungu akasema, kuitikia ombi lake: Tutakutia nguvu kwa kumtuma Harun. Na tutakupeni nyinyi wawili madaraka, na tutakuungeni mkono kwa miujiza. Kwa hivyo hawatoweza kukuvamieni. Na nyinyi wawili na walio kufuateni na wakaongoka kwa msaada wenu, mtakuwa wenye kuwashinda hawa makafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Akamwambia Mûsã, «Tutakupa nguvu kwa ndugu yako, na tutawapa nyinyi wawili hoja juu ya Firáwn na watu wake wasiweze kuwafikia nyinyi kwa ubaya wowote. Nyinyi wawili na wale wenye kuwaamini nyinyi ndio mtakaopewa ushindi juu ya Firáwn na watu wake, kwa sababu ya aya zetu na ukweli unaoonyeshwa na hizo aya».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net