Al-Qasas 28:31
القصصوَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَلَمَّا رَءَاهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَآنٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَـٰمُوسَىٰٓ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ ۖ إِنَّكَ مِنَ ٱلْـَٔامِنِينَ
Na tupa chini fimbo yako. Basi alipoiona ikitikisika kama nyoka, akarudi nyuma wala hakutazama. (Akaambiwa), "Ewe Musa, njoo mbele wala usihofu. Hakika wewe ni miongoni mwa walio katika amani."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tupa chini fimbo yako. Basi alipo iona ikitikisika kama nyoka, akarudi nyuma wala hakutazama. (Akaambiwa): Ewe Musa! Njoo mbele wala usiogope. Hakika wewe ni miongoni mwa walio salimika. [31]
[31] Na akanadiwa: Tupa chini fimbo yako. Akaitupa chini. Mwenyezi Mungu akaigeuza ikawa nyoka. Musa alipo iona inakwenda kama nyoka alikhofu, na akakimbia kwa kufazaika. Akaambiwa: Ewe Musa! Njoo, unaitwa urejee pahala pako, wala usiogope. Kwani wewe ni katika walio hifadhiwa na kila cha kuchukiza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwamba: «itupe fimbo yako!» Na Mûsã akaitupa, ikageuka kuwa nyoka anayetembea kwa haraka. Alipoiona inatetemeka kana kwamba ni nyoka kama walivyo nyoka wengine, aligeuka kumkimbia na hakugeuka kwa kuogopa. Na hapo Mola wake Alimuita, «Ewe Mûsã! Nielekee mimi, na usiogope! Wewe ni miongoni mwa wenye kusalimika na kila lenye kuchukiza».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net