Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 30

Al-Qasas 28:30

القصص

فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِىَ مِن شَـٰطِئِ ٱلْوَادِ ٱلْأَيْمَنِ فِى ٱلْبُقْعَةِ ٱلْمُبَـٰرَكَةِ مِنَ ٱلشَّجَرَةِ أَن يَـٰمُوسَىٰٓ إِنِّىٓ أَنَا ٱللَّهُ رَبُّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Basi alipoufikia, aliitwa kutokea ng'ambo ya bonde la kuliani katika eneo lililobarikiwa kutoka kwenye mti, "Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi alipo ufikia aliitwa kutoka ng'ambo ya bonde la kuliani katika eneo lilio barikiwa kutoka kwenye mti: Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. [30]

[30] Musa alipo ufikia moto alio uona alisikia kutoka upande wa kulia kwenye mti wenye kumea katika eneo lilio barikiwa ubavuni mwa Mlima, wito wa juu ukisema: Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana anaye stahiki kuabudiwa isipo kuwa Yeye, Mwenye kuumba viumbe vyote na ni Mwenye kuvilinda na kuvihifadhi na kuvilea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi Mûsã alipoujia moto, Allah Mtukufu Alimuita kutoka upande wa bonde la mkono wa kulia wa Mûsã, katika ardhi iliyobarikiwa ya upande wa mti kwamba: «Ewe Mûsã! Mimi Ndiye Allah Mtukufu, Mola wa viumbe wote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net