Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 29

Al-Qasas 28:29

القصص

فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى ٱلْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِۦٓ ءَانَسَ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ ٱمْكُثُوٓا۟ إِنِّىٓ ءَانَسْتُ نَارًا لَّعَلِّىٓ ءَاتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ ٱلنَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ

Maana

Basi Musa alipotimiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande wa Mlima 'Turi. Akawaambia ahali zake, "Ngojeni! Hakika mimi nimeona moto. Labda nitawaletea kutoka huko habari au kijinga cha moto ili mpate kuota moto."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi alipo timiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande wa Mlima T'uri. Akawaambia ahali zake: Ngojeni! Mimi nimeona moto, labda nitakuleteeni kutoka huko khabari au kijinga cha moto ili mpate kuota moto. [29]

[29] Musa alipo timiza muda wake walio patana, na akawa mume wa binti wa yule aliye mpokea, na akawa anarudi Misri, aliona njiani mwake katika upande wa Mlima wa T'uri moto unawaka. Akawaambia walio kuwa pamoja naye: Kaeni hapa. Mimi nimeuona moto, nimefurahi nao katika giza hili. Nitawendea nikuleteeni khabari ya njia, au nipate kijinga cha moto mpate walau moto wa kuota kujilinda na baridi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi Nabii wa Allah Mtukufu Mûsã, amani imshukie, alipomtekelezea mwenzake kipindi cha miaka kumi, nao ni muda mkamilifu zaidi wa vile vipindi viwili, na akaenda na watu wa nyumbani kwake kuelekea Misri, aliona moto upande wa jabali la Ṭūr. Mûsã alisema kuwaambia watu wa nyumbani kwake, «Subirini na mngojee. Mimi nimeona moto. Huenda nikawaletea habari kutoka kule, au nikawaletea kinga cha moto mkapata kujiotesha nacho».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net