Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 32

Al-Qasas 28:32

القصص

ٱسْلُكْ يَدَكَ فِى جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَآءَ مِنْ غَيْرِ سُوٓءٍ وَٱضْمُمْ إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ ٱلرَّهْبِ ۖ فَذَٰنِكَ بُرْهَـٰنَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦٓ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَـٰسِقِينَ

Maana

Ingiza mkono wako kwenye mfuko wako, utatoka mweupe pasipo na ubaya wowote. Na jiambatishe mkono wako ukihisi hofu. Basi hizi ni hoja mbili zitokazo kwa Mola wako Mlezi umpelekee Firauni na wakuu wa umma wake. Hakika hao walikuwa watu wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ingiza mkono wako kwenye mfuko wako, utatoka mweupe pasipo na ubaya. Na jiambatishe mkono wako ukihisi khofu. Basi hizi ni dalili mbili zitokazo kwa Mola wako Mlezi kumpelekea Firauni na wakuu wa umma wake. Hakika hao walikuwa watu mafaasiki. [32]

[32] Na uingize mkono wako kwenye uwazi wa nguo yako utatoka mweupe, bila ya ila wala maradhi. Na jiambatishe mkono wako ubavuni mwako katika nguo ukiwa una khofu. Wala usishituke kwa kuona fimbo imekuwa nyoka, na kuona mkono wako umekuwa mweupe. Kwani miujiza hii miwili inatokana na Mwenyezi Mungu ya kumkabili nayo Firauni na kaumu yake watapo ukabili Ujumbe wako kwa kuukadhibisha na hali wametoka kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tia mkono wako kwenye uwazi wa kanzu yako uliofunguliwa kifuani na uutoe, utatoka kuwa mweupe, kama barafu, ambao si wa ugonjwa wala mbalanga, na ujikumbatie kwa mikono yako ili usalimike na hofu. Hivi viwili nilivyokuonesha, ewe Mûsã, vya fimbo kugeuka nyoka na kuufanya mkono wako kuwa mweupe na wenye kung’ara, si kwa ugonjwa wala mbalanga, ni dalili mbili kutoka kwa Mola wako, uende nazo kwa Firáwn na viongozi wa watu wake. Hakika Firáwn na viongozi walio karibu naye walikuwa ni wakanushaji.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net