Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 27 · Aya ya 60

An-Naml 27:60

النمل

أَمَّنْ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَنۢبَتْنَا بِهِۦ حَدَآئِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنۢبِتُوا۟ شَجَرَهَآ ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ

Maana

Au ni nani yule aliyeziumba mbingu na ardhi, na akawateremshia maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamkuwa na uwezo wa kuiotesha miti yake. Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni kaumu waliopotoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka. [60]

[60] Bali, ewe Mtume, waulize: Ni nani aliye ziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake, na akakuteremshieni kutoka mbinguni mvua yenye manufaa, na kwa hiyo akakuotesheeni bustani nzuri zenye kupendeza. Msingeli weza nyinyi kuiotesha miti yake ya namna mbali mbali, na rangi mbali mbali, na matunda mbali mbali! Mipango hii iliyo umana sawa katika uumbaji inathibitisha kuwa hapana mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Lakini makafiri ni watu walio potoka wakaiacha Haki na Imani, na wameelekea kwenye upotovu na ushirikina.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waulize wao, «Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na Akawateremshia maji kutoka mbinguni, Akaotesha kwa hayo maji mabustani yenye mandhari mazuri?» Hamkuwa nyinyi ni wenye kuipanda miti yake lau si Allah Mtukufu kuwateremshia maji kutoka mbinguni. Kumuabudu Allah Mtukufu ndio ukweli na kumuabudu asiyekuwa Yeye ndio urongo. Je, kuna muabidiwa pamoja na Allah Mtukufu alifanya vitendo hivi mpaka aabudiwe pamoja na Yeye na ashirikishwe na Yeye? Bali washirikina hawa ni watu wanapotoka na njia ya haki na Imani, ndio wakamfanya Allah Mtukufu ni sawa na asiyekuwa Yeye katika kuabudiwa na kutukuzwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naml

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net