An-Naml 27:61
النملأَمَّن جَعَلَ ٱلْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَـٰلَهَآ أَنْهَـٰرًا وَجَعَلَ لَهَا رَوَٰسِىَ وَجَعَلَ بَيْنَ ٱلْبَحْرَيْنِ حَاجِزًا ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Au nani yule aliyeifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kizuizi? Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui. [61]
[61] Bali waulize, ewe Mtume: Nani aliye itengeneza ardhi hata ikafaa kukaliwa na watu wakatulia humo, na akaumba mito kati yake, na juu yake akaumba milima kuizuilia isiyumbe yumbe, na akayatenganisha maji matamu na maji ya chumvi hata yasichanganyike? Hapana mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kuumba peke yake. Lakini wengi wa watu hawanafiiki na ujuzi wa Haki kama ilivyo. Wamekuwa kama kwamba hawajui kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, kuviabudu vile mnavyovishirikisha na Mola wenu ni bora au Yule Aliyewafanyia ardhi kuwa ni mahali pa kutulia, Akaitoa mito kati yake, Akaiwekea majabali yaliyojikita na Akaweka kizuizi baina ya bahari mbili, ya tamu na chumvi, ili mojawapo isiiharibu nyingine? Je kuna muabudiwa yoyote pamoja na Allah Mtukufu alifanya hilo hata mumshirikishe na Yeye katika kuabudu kwenu? Bali wengi wa hawa washirikina hawajui kadiri ya ukubwa wa Allah Mtukufu, hivyo basi wanamshirikisha Yeye kwa kuiga na kwa udhalimu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net