Al-Furqaan 25:59
الفرقانٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ۚ ٱلرَّحْمَـٰنُ فَسْـَٔلْ بِهِۦ خَبِيرًا
Ambaye aliziumba mbingu na ardhi, na vilivyo kati yake kwa siku sita. Kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi. Mwingi wa rehema (Arrahman)! Uliza habari zake kwa amjuaye.[1]
[1] Yaani, muulize Mwenyezi Mungu mwenyewe ambaye anajua kila kitu, na hakuna kinachofichika kwake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
. Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye. [59]
[59] Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao kwa siku sita. Naye ametawala juu ya A'rshi, Kiti cha Enzi, cha Ufalme wote, na madaraka yake yameenea kila kitu. Na Yeye ndiye Mwingi wa Rehema, Arrahman. Na ukitaka lolote katika sifa zake muulize ajuae atakujibu. Naye ni Mwenyezi Mungu Mwenye hikima. "Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Ulize khabari zake kwa wamjuaye." Hizo Siku Sita ni usemi wa Mwenyezi Mungu, Mtukufu Aliye tukuka, kueleza wakati. Na Yeye Mtukufu ndiye Mwenye kujua zaidi kipimo cha hiyo Siku. Na kwa upande wa kiilimu za sayansi kazi ya kuumba ulimwengu unahitaji kupita vipindi na viwango mbali mbali. Na "Mbingu na ardhi na viliomo ndani yake" ni ishara ya vyombo vyote vya mbinguni, nyota, majua, sayari, miezi, mavumbi, gesi za namna mbali mbali, na nishat'i, Energy , na vyote hivyo vinavyo fanya ndio ulimwengu wa duniani na angani. Na kwa kuupanga ulimwengu wote, yaani uumbaji wote, kwa tafsili ya ukamilifu inayo kusanya kila kitu, ndio inaweka wazi, Utawala wa Mwenyezi Mungu, Subhanahu juu ya ulimwengu kwa jumla na kwa tafsili. "Uliza khabari zake kwa ajuaye". Katika kifungu hichi cha Aya hii tukufu pana uwongozi wa kisayansi kutokana na Mwenyezi Mungu kuonyesha dharura ya uchunguzi na utafiti wa mambo yanayo onekana ya uumbaji na mipango yake tuyaangalie ya ndani, ili tujue siri za uweza wa Mwenyezi Mungu katika kuanzisha huu ulimwengu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake kwa Siku sita, kisha akawa juu ya ʻArshi yake kulingana na utukufu Wake, Yeye Ndiye Mwingi wa rehema. Basi muulize, ewe Mtume, Mtambuzi kuhusu Yeye Allah Mtukufu, Aliyetakasika, Anajikusudia Mwenyewe Aliyetukuka, kwani Yeye Ndiye Anayejua sifa Zake, ukuu Wake na utukufu Wake. Na hakuna yoyote, katika binadamu, anayemjua zaidi Allah Mtukufu wala anayetambua habari Zake zaidi kuliko mja Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net