Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 60

Al-Furqaan 25:60

الفرقان

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱسْجُدُوا۟ لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا۟ وَمَا ٱلرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩

Maana

Na wanapoambiwa: Msujudieni Arrahman (Mwingi wa rehema!) Wao husema: Ni nani Arrahman (Mwingi wa rehema)? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe tu? Na huwazidishia kujitenga mbali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo ambiwa: Msujudieni Arrahman! Wao husema: Ni nani Arrahman? Je! Tumsujudie unaye tuamrisha wewe tu? Na huwazidishia chuki. [60]

[60] Na wakiambiwa hawa makafiri: Mnyenyekeeni Arrahmani, Mwingi wa Rehema, na mumuabdu, wao husema: Nani huyo Arrahmani? Sisi hatumjui, hata tumsujudie. Basi tukufuate amri yako tu? Na wanazidi kuwa mbali na kutengeka na Imani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakiambiwa makafiri, «Msujudieni Al-Raḥmān (Mwingi wa rehema) na muabuduni,» wanasema, «Hatumjui Al-Raḥmān (Mwingi wa rehema). Je, tukisujudie kila unachotuamrisha kukisujudia kwa kutii amri yako?» Basi hilo la kuwaita wao kumsujudia Al-Raḥmān (Mwingi wa rehema) linawaongezea wao kuikimbia imani na kuwa mbali nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net