Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 58

Al-Furqaan 25:58

الفرقان

وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱلْحَىِّ ٱلَّذِى لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِۦ ۚ وَكَفَىٰ بِهِۦ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرًا

Maana

Na mtegemee aliye Hai, ambaye hafi. Na umtakase kwa sifa zake. Naye anatosha kuwa ndiye Mwenye habari zote za dhambi za waja wake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mtegemee Aliye Hai, ambaye hafi. Na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kwake kuwa yeye ni Mwenye khabari za dhambi za waja wake. [58]

[58] Na katika mambo yako mtegemee Mwenyezi Mungu Aliye Hai, ambaye hayumkini kufa. Na mtakase na mtukuze kwa kuzisifu neema zake. Na waachilie mbali walio toka kwenye Njia. Kwani Mwenyezi Mungu anawajua vyema, na atawalipa kwa dhambi zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na jitegemeze kwa Allah Mtukufu Ambaye Ana uhai uliokamilika kwa namna zote, kama inavyonasibiana na utukufu Wake, Ambaye hafi, na umtakase na sifa za upungufu. Na inatosha kuwa Allah Mtukufu ni Mtambuzi wa madhambi ya viumbe Vyake. Hakuna chochote kinachofichika Kwake katika hayo. Na Atawahesabia na Atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net