Al-Furqaan 25:57
الفرقانقُلْ مَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِلَّا مَن شَآءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
Sema: Sikuwaomba ujira wowote juu yake; isipokuwa atakaye na ashike njia iendayo kwa Mola wake Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Sikukuombeni ujira juu yake; ila atakaye na ashike njia iendayo kwa Mola wake Mlezi. [57]
[57] Na waambie: Hakika mimi sitafuti kwa huku kukuiteni muufuate Uislamu ujira wowote wala malipo. Ila nilitakalo ni mwongoke na muifuate Njia ya Haki mrejee kwa Mola wenu Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, «Sitaki kutoka kwenu, kwa kufikisha ujumbe, malipo yoyote. Lakini mwenye kutaka kuongoka na kufuata njia ya haki inayompeleka kwa Mola wake na kutenda katika mambo Anayoyaridhia, mimi sitawalazimisha hilo, isipokuwa hilo, kwa kweli, ni bora kwa maslahi ya nafsi zenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net