Al-Furqaan 25:56
الفرقانوَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا
Nasi hatukukutuma isipokuwa uwe Mbashiri na Mwonyaji.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nasi hatukukutuma ila kuwa ni Mbashiri na Mwonyaji. [56]
[56] Na ewe Nabii! Huna jukumu ila kufikisha hayo ulio tumwa basi, na kuwabashiria Pepo Waumini, na kuwakhofisha makafiri kwa haya watayo yakuta. Baada ya hayo huna jengine unalo takiwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukukutuma wewe, ewe Mtume, isipokuwa uwe ni mwenye kuwabashiria Waumini Pepo na mwenye kuwaonya makafiri na Moto.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net