Al-Furqaan 25:51
الفرقانوَلَوْ شِئْنَا لَبَعَثْنَا فِى كُلِّ قَرْيَةٍ نَّذِيرًا
Na tungelitaka, tungelituma katika kila mji Mwonyaji.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tungeli taka tungeli peleka katika kila mji Mwonyaji. [51]
[51] Na lau kuwa tumetaka basi tungeli mpeleka mwonyaji kwenye kila mji. Basi jitahidi na wito wako; na wacha maneno ya makafiri; na tupilia mbali wanayo yaleta.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau tungetaka tungepeleka muonyaji katika kila mji, wa kuwalingania wao kwa Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, na kuwaonya wao na adhabu Yake. Lakini tumekufanya wewe, ewe Mtume, ni mwenye kupelekwa kwa watu wote wa ardhini, na tumekuamrisha wewe uwafikishie hii Qur’ani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net