Al-Furqaan 25:50
الفرقانوَلَقَدْ صَرَّفْنَـٰهُ بَيْنَهُمْ لِيَذَّكَّرُوا۟ فَأَبَىٰٓ أَكْثَرُ ٱلنَّاسِ إِلَّا كُفُورًا
Na kwa yakini tumeibadilibadili kati yao wapate kukumbuka. Lakini wengi wa watu wanakataa isipokuwa kukufuru tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa yakini tumeisarifu kati yao wapate kukumbuka. Lakini watu wengi wanakataa ila kukufuru. [50]
[50] Na hii Qur'ani tumeibainisha na tumeisarifu, tumeifanya, ili watu wamkumbuke Mola wao Mlezi, na wawaidhike, na watende kwa mujibu wake. Lakini wengi wa watu wanakataa isipo kuwa ukafiri na inda tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakika tunateremsha mvua juu ya sehemu ya ardhi bila ya nyingine, ili wale walioteremshiwa mvua wapate kukumbuka neema ya Allah Mtukufu juu yao na wamshukuru, na ili wale walionyimwa mvua wafanye haraka kutubia kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, Apate kuwarehemu wao na kuwanywesha. Lakini wengi wa watu wanakataa na wanakanusha neema zetu juu yao, kama neno lao wanalolisema, «tumeletewa mvua kwa sababu ya nyota kadha na kadha».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net