Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 49

Al-Furqaan 25:49

الفرقان

لِّنُحْـِۧىَ بِهِۦ بَلْدَةً مَّيْتًا وَنُسْقِيَهُۥ مِمَّا خَلَقْنَآ أَنْعَـٰمًا وَأَنَاسِىَّ كَثِيرًا

Maana

Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyokufa, na tuwanyweshe wanyama na watu wengi tuliowaumba.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyo kufa, na tuwanyweshe wanyama na watu wengi tulio waumba. [49]

[49] Tunaiteremsha mvua kwa sababu makulima yapate kumea na kukua, na ardhi ipate kufufuka baada ya kufa kwake, na wanyweshwe watu na wanyama walio umbwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ili tutoe kwayo mimea mahali pasipo na mimea, ipate kuhuika ardhi ya ukame baada ya kuwa imekufa (kwa ukavu), na ili tuwanyweshe maji hayo wanyama howa na watu miongoni mwa viumbe vyetu vyingi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net