Al-Furqaan 25:48
الفرقانوَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ ٱلرِّيَـٰحَ بُشْرًۢا بَيْنَ يَدَىْ رَحْمَتِهِۦ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً طَهُورًا
Naye ndiye anayezituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naye ndiye anaye zituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi. [48]
[48] Na Yeye ndiye aliye zifanya pepo zimtumikie, zikasukuma mawingu, nayo yakawabashiria watu itakuja mvua, ambayo ni rehema itokayo kwake kuwaendea wao. Na hakika Sisi tunateremsha kutoka mbinguni maji safi yanayo safisha kuondoa najisi na uchafu. "Na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi." Katika Aya hii tukufu Mwenyezi Mungu anawasimbulia watu kwa kuwateremshia maji yaliyo safi kutoka mbinguni. Na Aya hii inafahamisha kuwa maji ya mvua katika asli ya kuumbwa kwake ni maji safi kabisa. Na juu ya kuwa baada yake yanabeba takataka nyingi katika anga, lakini bado yamo katika daraja ya usafi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Yeye Ndiye Aliyetuma upepo unaobeba mawingu, wenye kuwabashiria watu mvua, ikiwa ni rehema kutoka Kwake; na tumeyateremsha kutoka mbinguni maji ya kujisafisha nayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net