Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 52

Al-Furqaan 25:52

الفرقان

فَلَا تُطِعِ ٱلْكَـٰفِرِينَ وَجَـٰهِدْهُم بِهِۦ جِهَادًا كَبِيرًا

Maana

Basi usiwatii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi usiwat'ii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa. [52]

[52] Na endelea na kulingania kwako kwa Haki, na kufikisha Ujumbe wa Mola wako Mlezi. Na wao wakiupinga wito wako, na wakawavamia Waumini basi wapige vita, na kwa hayo pigana Jihadi kubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi usiwatii makafiri kwa kuacha kitu chochote kile ambacho umetumwa nacho. Lakini fanya bidii yako katika kuufikisha ujumbe na upigane jihadi na wenye kuikanusha hii Qur’ani, kupigana jihadi kukubwa kusikochanganyika na udhaifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net