Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 5

Al-Furqaan 25:5

الفرقان

وَقَالُوٓا۟ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ ٱكْتَتَبَهَا فَهِىَ تُمْلَىٰ عَلَيْهِ بُكْرَةً وَأَصِيلًا

Maana

Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyoviandikisha, anavyosomewa asubuhi na jioni.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyo viandikisha, anavyo somewa asubuhi na jioni. [5]

[5] Wakaisema Qur'ani pia kuwa ati ni uwongo walio andika watu wa kale katika vitabu vyao, kisha akawataka wao wamuandikie na wamsomee asubuhi na jioni mpaka ahifadhi na apate kusema naye hayo hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na walisema kuhusu Qur’ani, «Hiyo ni hadithi za wakale katika vitabu vyao, na Muhammad amezinakili. Basi hizo anasomewa asubuhi na jioni,»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net