Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 43

Al-Furqaan 25:43

الفرقان

أَرَءَيْتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَـٰهَهُۥ هَوَىٰهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا

Maana

Je, umemwona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake? [43]

[43] Ewe Mtume! Umeona upotovu wa mwenye kufuata matamanio yake na pumbao lake hata akawa anaabudu mawe ambayo hayadhuru wala hayanafiishi? Na wewe umetumwa uwe mwonyaji na mbashiri, wala hukuwakilishwa kwa imani yao na uwongofu wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwangalie, ewe Mtume, kwa kumuonea ajabu yule aliyeyatii matamanio yake kama kumtii Allah Mtukufu. Je, wewe utakuwa ni mwenye kumtunza mpaka umrudishe kwenye Imani?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net