Al-Furqaan 25:44
الفرقانأَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَٱلْأَنْعَـٰمِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا
Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao sio isipokuwa ni kama wanyama tu, bali wao wamepotea zaidi njia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia. [44]
[44] Na hivyo unadhani kuwa wengi wao wanasikia kwa sikio la kufahamu au wanaongoka kwa akili zao? Wamesha tupilia mbali kama walivyo amrishwa na ndoto zao. Wamekuwa kama wanyama wa kufuga, hawanalo linalo washughulisha ila kula, na kunywa, na kustarehe na maisha ya dunia. Wala hawana fikra yoyote baada ya hayo. Bali hali yao ni ovu zaidi kuliko ya wanyama, kwani wanyama huwafuata bwana zao katika yenye kheri nao, na wanayaepuka ya kuwadhuru. Lakini watu hawa wanajitokomeza wenyewe kwenye mambo ya kuwahiliki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au unadhani kwamba wengi wao wanazisikia aya za Allah Mtukufu, kusikia kwa kuzingatia, au wanayaelewa yaliyomo ndani yake? Hawakuwa isipokuwa ni kama wanyama, katika kutonufaika kwa wanayoyasikia, bali wao wamepotea njia zaidi kuliko hao wanyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net