Al-Furqaan 25:42
الفرقانإِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنْ ءَالِهَتِنَا لَوْلَآ أَن صَبَرْنَا عَلَيْهَا ۚ وَسَوْفَ يَعْلَمُونَ حِينَ يَرَوْنَ ٱلْعَذَابَ مَنْ أَضَلُّ سَبِيلًا
Kwa hakika alikuwa karibu zaidi kutupoteza tuiache miungu yetu, lau kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapoiona adhabu, ni nani aliyepotea zaidi njia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika alikuwa karibu kutupoteza tuiache miungu yetu, ingeli kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapo iona adhabu, ni nani aliye potea njia. [42]
[42] Mtu huyu hakika kajaaliwa kuwa na ufasihi mzuri, na hoja za kuvutia kwa wanao msikia. Na hapana shaka ameweza kuchota katika imani zetu hata alikaribia kututoa kwa miungu yetu tumfuate mungu wake. Lakini sisi tumesimama imara juu miungu yetu na dini yetu. (Mwenyezi Mungu anasema:) Tutakuja wabainishia ukweli wa mambo watapo kuja iona adhabu Siku ya Kiyama, na watajua nani huyo aliye thibiti katika upotovu na makosa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yeye amekaribia kutuepusha na kuwaabudu masanamu wetu kwa hoja zake za nguvu na ufasaha wake, lau Tusingesimama imara juu ya kuwaabudu. Na watajuwa, watakapoiona adhabu wanayoistahili, ni nani aliyepotoka zaidi kidini: ni wao au ni Muhammad?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net