Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 39

Al-Furqaan 25:39

الفرقان

وَكُلًّا ضَرَبْنَا لَهُ ٱلْأَمْثَـٰلَ ۖ وَكُلًّا تَبَّرْنَا تَتْبِيرًا

Maana

Na wote tuliwapigia mifano, na wote tuliwaangamiza kabisa kabisa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wote tuliwapigia mifano, na wote tuliwaangamiza kabisa kabisa. [39]

[39] Na Sisi tumezionya kaumu zote hizi. Tukawakumbusha mawaidha, na mifano ya kweli yenye manufaa. Lakini hawakuwaidhika. Tukawashika wote kwa kuwaadhibu, tukawahiliki, na tukayabomoa majumba yao mpaka kifusi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ummah wote hao tuliwabainishia hoja na kuwafafanulia dalili na tukawaondolea nyudhuru (za kutojua). Pamoja na hivyo, hawakuamini, na kwa ajili hiyo tuliwapa maangamivu kwa kuwaadhibu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net