Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 38

Al-Furqaan 25:38

الفرقان

وَعَادًا وَثَمُودَا۟ وَأَصْحَـٰبَ ٱلرَّسِّ وَقُرُونًۢا بَيْنَ ذَٰلِكَ كَثِيرًا

Maana

Na (tuliwaangamiza) kina 'Adi na Thamudi na watu wa Rass na vizazi vingi vilivyokuwa kati yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tuliwaangamiza kina A'di na Thamudi na watu wa Rass na vizazi vingi vilivyo kuwa kati yao. [38]

[38] Na kadhaalika tuliwahiliki A'di na Thamudi na watu wa Rass walipo wakanusha Mitume wao. Na tuliziangamiza kaumu nyingi baina ya kaumu ya Nuhu na baina ya A'di, yakawapata malipo ya wenye kudhulumu. Rass, kama ilivyo elezwa katika Mufradaat ya Raaghib Al-As'fahani, ni bonde, na akatolea ushahidi ubeti wa shairi: (Nao ni bonde la Rass, kama mkono kwa mdomo.) Hao watu wa Rass, kama ilivyo kuja katika Aya tukufu, ni watu walio kuwa wakiabudu masanamu. Mwenyezi Mungu aliwatumia Shuaib. Basi hao ndio walio pelekewa Mtume Shuaib a.s. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika amewaeleza hao kaumu ya Shuaib kuwa ni Watu wa Vichakani (Al-Aykat), napo ni pahali penye miti mingi panasifika kwa neema, na mara nyengine wanaitwa Watu wa Rass, nalo ni bonde lenye kheri kubwa, kuonesha neema alizo waneemesha Mwenyezi Mungu. Nao wakazikufuru neema za Mwenyezi Mungu, wakaabudu masanamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tuliwaangamiza hao ‘Ᾱd, watu wa Hūd, na Thamūd, watu wa Ṣāliḥ, na watu wa Kisimani na watu wengine wengi waliokuwako baina ya watu wa Nûḥ, kina ‘Ãd, kina Thamūd na watu wa Rass(hapo kisimani), hakuna awajuao isipokuwa Allah Mtukufu. 1 Dalili ya umola wa Allah Mtukufu ni dalili ya kuw

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net