Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 37

Al-Furqaan 25:37

الفرقان

وَقَوْمَ نُوحٍ لَّمَّا كَذَّبُوا۟ ٱلرُّسُلَ أَغْرَقْنَـٰهُمْ وَجَعَلْنَـٰهُمْ لِلنَّاسِ ءَايَةً ۖ وَأَعْتَدْنَا لِلظَّـٰلِمِينَ عَذَابًا أَلِيمًا

Maana

Na kaumu ya Nuhu, walipowakanusha Mitume, tuliwazamisha, na tukawafanya ni Ishara kwa watu. Na tumewaandalia madhalimu adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watu wa Nuhu, walipo wakanusha Mitume, tuliwazamisha, na tukawafanya ni Ishara kwa watu. Na tumewaandalia wenye kudhulumu adhabu chungu. [37]

[37] Hali kadhaalika kabla ya Musa tuliwafanyia kaumu ya Nuhu walipo mkadhibisha, na aliye mkanusha Mtume mmoja basi amewakanusha Mitume wote. Nao tukawazamisha katika tufani, na tukawafanya wawe ni zingatio kwa watu. Na tukawajaalia hao na kila mshirikina kupata adhabu chungu Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tuliwazamisha watu wa Nûḥ kwa mafuriko walipomkanusha. Na mwenye kumkanusha Mtume yoyote huwa amewakanusha Mitume wote. Na tulikufanya kule kuwazamisha ni mazingatio kwa watu. Na tutawapatia wao na wale waliofuata njia yao katika kukanusha, Siku ya Kiyama, adhabu yenye kuumiza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net