Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 36

Al-Furqaan 25:36

الفرقان

فَقُلْنَا ٱذْهَبَآ إِلَى ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا فَدَمَّرْنَـٰهُمْ تَدْمِيرًا

Maana

Tukawaambia: "Nendeni kwa kaumu waliokanusha Ishara zetu." Basi tukawateketeza kabisa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

. Tukawaambia: Nendeni kwa watu walio kanusha Ishara zetu. Basi tukawateketeza kabisa. [36]

[36] Tukasema: Nenda wewe na nduguyo kwa Firauni na watu wake. Tukamuunga mkono kwa miujiza inayo onyesha ukweli wake. Hawakumuamini, wakamkadhibisha. Mwisho wao ukawa tukawateketeza na tukawafutilia mbali!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tukawaambia wao wawili, «nendeni kwa Fir’̔awn na watu wake waliozikanusha dalili za umola(1) wetu na uungu wetu.» Basi wakawaendea na wakawalingania wamuamini Allah Mtukufu, wamtii na wasimshirikishe. Wakawakanusha, na kwa hivyo tukawaangamiza maangamivu makubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net