Al-Furqaan 25:40
الفرقانوَلَقَدْ أَتَوْا۟ عَلَى ٱلْقَرْيَةِ ٱلَّتِىٓ أُمْطِرَتْ مَطَرَ ٱلسَّوْءِ ۚ أَفَلَمْ يَكُونُوا۟ يَرَوْنَهَا ۚ بَلْ كَانُوا۟ لَا يَرْجُونَ نُشُورًا
Na kwa yakini wao walikwisha ujia mji ulioteremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiuona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa yakini wao wanafika kwenye nchi ilio teremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiiona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa. [40]
[40] Na hawa Makureshi katika safari zao za kwenda Sham wanapita kwenye mji wa kaumu Lut'i, tulio unyeshea mvua ya shari na ovu kabisa, nayo ni mawe ya Motoni. Je! Hawauoni mji huo wakawaidhika kwa yaliyo wafika watu wake? Hakika wao wanauona huo, lakini si kwa macho ya kuwaidhika na kuzingatia. Kwani hawaamini ahadi (za Mwenyezi Mungu) wala kufufuliwa. Wala hawataraji kuwa ipo siku watakuja fufuliwa kwa ajili ya hisabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na washirikina wa Makkah walikuwa wakikipitia kijiji cha watu wa Lūṭ katika safari zao, nacho ni kijiji cha Sadūm ambacho kiliangamizwa kwa mawe kutoka mbinguni, wasizingatie kwa hilo, bali walikuwa hawatazamii kuwa kuna marejeo Siku ya Kiyama ambapo wao watalipwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net