Al-Furqaan 25:31
الفرقانوَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِىٍّ عَدُوًّا مِّنَ ٱلْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا
Na vivyo hivyo tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wahalifu, na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na vivi hivi tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wakosefu, na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru. [31]
[31] Kama tulivyo wajaalia watu wako, ewe Muhammad, wanavyo kufanyia uadui na kukukadhibisha, basi kadhaalika tulimjaalia kila Nabii ana maadui miongoni mwa wakosefu, wanao mfanyia uadui na wanaupinga wito wake. Na Mwenyezi Mungu atakunusuru, na atakuongoa mpaka uwashinde. Na Yeye anakutosha kwa uwongofu na kukunusuru.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kama tulivyokufanya, ewe Mtume, uwe na maadui miongoni mwa wahalifu wa watu wako, tulimfanya kila Nabii, miongoni mwa Manabii, awe na adui kati ya wale wahalifu wa watu wake. Basi vumilia kama walivyovumilia. Na inatosha kuwa Mola wako ni Mwenye kuongoa, ni Mwenye kuelekeza, ni Mwenye kuonyesha njia, na ni Mwenye kutoa msaada wa kukusaidia wewe dhidi ya maadui zako. Katika haya pana maliwazo kwa Nabii Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net