Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 30

Al-Furqaan 25:30

الفرقان

وَقَالَ ٱلرَّسُولُ يَـٰرَبِّ إِنَّ قَوْمِى ٱتَّخَذُوا۟ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ مَهْجُورًا

Maana

Na Mtume alikuwa akisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika kaumu yangu wameifanya hii Qur-ani kuwa ni kihame.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni kihame. [30]

[30] Na Mtume alisema akimshitakia Mwenyezi Mungu kwa taabu anazo zipata kwa watu wake: Hakika hawa wameiacha Qur'ani na wameihama, na wameshikilia katika kuipuuza, na kuifanyia inda na uadui.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Mtume amesema akishtakia matendo ya watu wake, Ewe Mola wangu! Kwa kweli watu wangu wameiacha hii Qur’ani na wameihama, wameendelea sana katika kuipa mgongo na kuacha kuizingatia na kuitumia na kuifikisha. Katika aya hii pana onyo kali kwa anayeihama Qur’ani na kutoifanyia kazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net