Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 29

Al-Furqaan 25:29

الفرقان

لَّقَدْ أَضَلَّنِى عَنِ ٱلذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَآءَنِى ۗ وَكَانَ ٱلشَّيْطَـٰنُ لِلْإِنسَـٰنِ خَذُولًا

Maana

Hakika alinipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shetani ni haini mkubwa kwa mwanadamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shet'ani ni khaini kwa mwanaadamu. [29]

[29] Rafiki huyu amenibaidisha na Ukumbusho, Dhikr, kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuikumbuka Qur'ani baada ya kwisha kuwa ni nyepesi kwangu. Ndio hivi Shetani anavyo mkhini binaadamu, na kumtokomeza kwenye hilaki yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Amenipoteza rafiki huyu na kuniepusha na Qur’ani baada ya kunijia, Na Shetani aliyefukuzwa kwenye rehema za Allah Mtukufu amekuwa daima ni mwenye kumtupa mwanadamu. Katika aya hizi kuna onyo kwamba rafiki mbaya asifuatwe, kwani yeye huenda akawa ni sababu ya kumtia, yule anayefuatana na yeye, Motoni.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net