Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 32

Al-Furqaan 25:32

الفرقان

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ ٱلْقُرْءَانُ جُمْلَةً وَٰحِدَةً ۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِۦ فُؤَادَكَ ۖ وَرَتَّلْنَـٰهُ تَرْتِيلًا

Maana

Na wakasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur-ani yote mara moja tu? Hayo ni hivyo ili tuuimarishe kwayo (ufahamu wa) moyo wako, na ndiyo tumeisoma kwa mafungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur'ani kwa jumla moja? Hayo ni hivyo ili tuuthibitishe moyo wako, na ndio tumeisoma kwa mafungu. [32]

[32] Na makafiri kutaka kuikebehi Qur'ani walisema: Kwa nini haikuteremshwa kwa mara moja? Na Sisi hakika tumeiteremsha kwa mapande mapande ili moyo wako uthibiti kwayo kwa raha yako na ili uihifadhi. Na tumeisoma, yaani tumeigawa kwa Aya, au tumeisoma kwa ulimi wa Jibril, kidogo kidogo kwa utulivu na upole.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Waliokanusha walisema, «Si hii Qur’ani ateremshiwe Muhammad kwa mara moja» kama ilivyokuwa Taurati, Injili na Zaburi? Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Akasema «Tumeiteremsha ikiwa hivyo, kidogo kidogo, ili kuutia nguvu moyo wako na ili wewe uzidi utulivu, upate kuielewa na kuibeba, na tumeifafanua kwa kuithibitisha na kwa kuileta polepole».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net