Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 23

Al-Furqaan 25:23

الفرقان

وَقَدِمْنَآ إِلَىٰ مَا عَمِلُوا۟ مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَـٰهُ هَبَآءً مَّنثُورًا

Maana

Na tutayaendea yale waliyoyatenda katika matendo na tuyafanye kama mavumbi yaliyotawanywa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama mavumbi yaliyo tawanyika. [23]

[23] Na Siku ya Kiyama tutawaletea waliyo yatenda katika mambo ya kuonyesha wema kwa dhaahiri na hisani katika dunia, na Sisi tutayafanya yaondokee patupu, na tutawaharimisha thawabu zake, kwa kuwa yamekosa Imani ambayo ni dharura ipatikane ili vitendo vitiwe maanani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo tutayaleta yale waliyoyafanya yanayoonekana kuwa ni mazuri na ya kidini, tuyafanye ni yenye kubatilika na kupotea. Hayatawanufaisha na yatakuwa ni kama vumbi linalorushwa, nalo ni lile vumbi lembamba linaloonekana kwenye mwangaza wa jua. Hivyo ni kwamba matendo mema hayawi na manufaa yoyote huko Akhera isipokuwa mwenye kuyafanya awe na imani ya kumuamini Allah Mtukufu na kumtakasia na kumfuata Mtume Wake Muhammd, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net