Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 24

Al-Furqaan 25:24

الفرقان

أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ يَوْمَئِذٍ خَيْرٌ مُّسْتَقَرًّا وَأَحْسَنُ مَقِيلًا

Maana

Watu wa Bustanini siku hiyo watakuwa katika makazi bora na mahali penye starehe nzuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watu wa Peponi siku hiyo watakuwa katika makaazi bora na mahali penye starehe nzuri. [24]

[24] Watu wa Peponi Siku ya Kiyama ndio watao kuwa na utulivu bora, na mashukio mazuri, na makaazi ya starehe, kwa sababu hii ni Pepo walio andaliwa Waumini, si Moto walio andaliwa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watu wa Peponi, Siku ya Kiyama, watakuwa na mahali pa kutulia bora zaidi kuliko watu wa Motoni, na watakuwa na mashukio mazuri kabisa. Raha yao imekamilika na starehe yao haitakuwa na chochote kile chenye kuharibu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net