Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 22

Al-Furqaan 25:22

الفرقان

يَوْمَ يَرَوْنَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ لَا بُشْرَىٰ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُجْرِمِينَ وَيَقُولُونَ حِجْرًا مَّحْجُورًا

Maana

Siku watakapowaona Malaika, hakutakuwa na furaha yoyote siku hiyo kwa wahalifu. Na watasema, "Mwenyezi Mungu apishe mbali!"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku watakayo waona Malaika haitakuwa furaha siku hiyo kwa wakosefu. Na watasema: Mungu apishe mbali! [22]

[22] Siku ya Kiyama watawaona Malaika kama walivyo tamani, na hayo yatakuwa ni sababu ya kitisho kwao wala si jambo la kuwafurahisha. Watatafuta kujilinda nao, kama walivyo kuwa wakitafuta kujilinda na vinavyo watisha duniani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Siku watakapowaona Malaika wakati wa kufa kwao, na wakiwa ndani ya makaburi yao na Siku ya Kiyama, kwa sura ambazo sizo zile walizozitaka, sio kuwapa bishara ya Pepo, lakini kuwaambia, «Allah Mtukufu Ameifanya Pepo ni mahali palipoharamishwa kwenu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net