Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 21

Al-Furqaan 25:21

الفرقان

وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْنَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَوْ نَرَىٰ رَبَّنَا ۗ لَقَدِ ٱسْتَكْبَرُوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِمْ وَعَتَوْ عُتُوًّا كَبِيرًا

Maana

Na walisema wale wasiotarajia kukutana nasi, "Mbona sisi hatukuteremshiwa Malaika au tumwone nasi Mola wetu Mlezi?" Hakika, hawa wamejiona bora nafsi zao; na wamepanda kichwa, vikubwa mno!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

NA WALISEMA wale wasio taraji kukutana nasi: Mbona sisi hatuteremshiwi Malaika au hatumwoni Mola wetu Mlezi? Kwa yakini hawa wamejiona bora nafsi zao, na wamepanda kichwa vikubwa mno! [21]

[21] Na wakasema wanao kataa kufufuliwa na wala hawatumai kuwa yapo malipo kwa vitendo vyao: Kwa nini hatuteremshiwi Malaika wa kukuunga mkono, au Mwenyezi Mungu akajionyesha kwetu na akatwambia kwamba kweli Yeye kakutuma? Kiburi kimewajaa katika nafsi zao, na wamepita mpaka katika udhalimu na ujabari!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na walisema wale ambao hawatarajii kukutana na Mola wao baada ya kufa kwao kwa kuwa wanamkanusha, «Si angalau tuteremshiwe Malaika watueleze kwamba Muhammad ni mkweli au tumuone Mola wetu waziwazi Atuelezee habari ya ukweli wake juu ya utume wake.» Kwa kweli wamejiona nafsi zao na wamefanya kiburi kwa kuwa wamefanya ujasiri kusema hili na wamepita mpaka katika ujeuri wao na ukafiri wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net