Al-Furqaan 25:20
الفرقانوَمَآ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ إِلَّآ إِنَّهُمْ لَيَأْكُلُونَ ٱلطَّعَامَ وَيَمْشُونَ فِى ٱلْأَسْوَاقِ ۗ وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا
Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa wakila chakula, na wakienda masokoni. Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni majaribio kwa wengine. Je, mtasubiri? Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa wakila chakula, na wakenda masokoni. Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni majaribio kwa wengine; je! Mtasubiri? Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuona. [20]
[20] Na ikiwa washirikina wanakutia ila ewe Nabii, kwa kula kwako chakula, na kwenda kwako masokoni kwa ajili ya kazi na kuchuma maisha, basi huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake walio kuja kabla yako. Hatukumtuma yeyote kati yao ila alikuwa akila chakula, na anakwenda kwenda masokoni. Na enyi watu! Tumewafanya baadhi yenu wawe ni mitihani kwa wenginewe. Na mafisadi wanafanya hila kuziba Njia ya Uwongofu na Haki kwa namna mbali mbali. Basi, enyi Waumini, mtavumilia juu ya Haki yenu, na mtaishikilia Dini yenu, mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake kwa ushindi? Subirini! Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvizunguka vitu vyote, na atamlipa kila mtu kwa kitendo chake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukumtuma yoyote kabla yako, ewe Mtume, miongoni mwa Mitume wetu, isipokuwa walikuwa binadamu, wanaokula chakula na wanaoenda sokoni. Na tumewafanya baadhi yenu, enyi watu, ni maonjo na mtihani kwa wengine, kwa uongofu na upotevu, utajiri na umasikini, uzima na ugonjwa. Basi je, mtavumilia msimame imara juu ya yale ambayo Allah Mtukufu Amewalazimisha nayo na mumshukuru ili Mola wenu awape malipo mema au hamtavumilia mustahili kuteswa? Na Mola wako, ewe Mtume, Anamuona anayepapatika au anayevumilia, na anayekanusha au anayeshukuru.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net