Al-Furqaan 25:19
الفرقانفَقَدْ كَذَّبُوكُم بِمَا تَقُولُونَ فَمَا تَسْتَطِيعُونَ صَرْفًا وَلَا نَصْرًا ۚ وَمَن يَظْلِم مِّنكُمْ نُذِقْهُ عَذَابًا كَبِيرًا
Basi waliwakanusheni kwa mliyoyasema. Kwa hivyo hamwezi kujiondolea wala kujisaidia. Na atakayedhulumu miongoni mwenu tutamwonjesha adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi walikukanusheni kwa mliyo yasema. Kwa hivyo hamwezi kujiondolea wala kujisaidia. Na atakaye dhulumu miongoni mwenu tutamwonjesha adhabu kubwa. [19]
[19] Wataambiwa wenye kuabudu, washirikina: Wamekukadhibisheni hao mlio kuwa mkiwaabudu, ambao mkidai kuwa wamekupotezeni. Basi nyinyi leo mnarejea kwenye adhabu. Hamna hila ya kuepukana nayo; wala hamyapati manusura ya kukutoeni. Na wajue waja wote kwamba mwenye kudhulumu kwa ukafiri na uasi kama walivyo fanya hao basi Sisi tutawaadhibu adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo waambiwe washirikina, «Kwa kweli, wamewakanusha nyinyi, hawa mliowaabudu kwenye madai yenu juu yao. Nyinyi hamuwezi kuzikinga nafsi zenu na adhabu wala kuziokoa. Na mwenye kumshirikisha Allah Mtukufu, akajidhulumu nafsi yake, akamuabudu asiyekuwa Allah Mtukufu na akafa katika hali hiyo, Allah Mtukufu Atamuadhibu adhabu kali».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net