Al-Furqaan 25:14
الفرقانلَّا تَدْعُوا۟ ٱلْيَوْمَ ثُبُورًا وَٰحِدًا وَٱدْعُوا۟ ثُبُورًا كَثِيرًا
Msiombe kufa mara moja tu, bali mfe mara nyingi!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Msiombe kufa mara moja tu, bali mfe mara nyingi! [14]
[14] Wataambiwa kwa kuwahizi na kuwakejeli: Msitake kuangamia mara moja tu, bali takeni muangamie mara nyingi. Hamtopata kusalimika na hayo mliyo nayo. Na hakika namna ya adhabu zao ni nyingi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo wataambiwa kwa kukatishwa tamaa, leo msijiombee maangamivu mara moja, lakini jiombeeni mara nyingi, kwani hilo halitawaongezea isipokuwa makero, hakuna chenye kuwaokoa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net