Al-Furqaan 25:13
الفرقانوَإِذَآ أُلْقُوا۟ مِنْهَا مَكَانًا ضَيِّقًا مُّقَرَّنِينَ دَعَوْا۟ هُنَالِكَ ثُبُورًا
Na watakapotupwa humo mahali penye dhiki, hali wamefungwa, wataomba wafe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na watakapo tupwa humo mahali dhiki, hali wamefungwa, wataombawafe. [13]
[13] Na watapo tupwa katika pahali pembamba kwa kulingana na unene wao, nao wamefungwa pingu mikono yao kwenye shingo zao, watapiga kelele kuhimiza wateketezwe upesi upesi ili wapate kupumzika na kitisho cha adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pindi wakitupwa katika mahali pembamba sana pa moto wa Jahanamu, ikiwa mikono yao imeshikanishwa na minyonyoro kwenye shingo zao, hapo watajiapiza kuangamia ili wajiokoe nayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net