Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 12

Al-Furqaan 25:12

الفرقان

إِذَا رَأَتْهُم مِّن مَّكَانٍۭ بَعِيدٍ سَمِعُوا۟ لَهَا تَغَيُّظًا وَزَفِيرًا

Maana

Ule Moto ukiwaona tangu mahali mbali, wao watasikia hasira yake na mngurumo wake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ule Moto ukiwaona tangu mahali mbali wao watasikia hasira yakena mngurumo wake. [12]

[12] Wakiuona Moto, na huo Moto ukawaona, wataisikia sauti yenye hasira, yenye hamu kuwateketeza. Na katika hayo ni mfano wa mingurumo inayo toka kifuani mwa aliye kasirika kuwa ni alama ya ukali alio nao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Moto huo ukiwaona hawa wakanushaji Siku ya Kiyama, kutoka mahali mbali, watasikia sauti ya kuchemka kwake na mkoromo wake kwa ukali wa hasira zake kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net