Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 15

Al-Furqaan 25:15

الفرقان

قُلْ أَذَٰلِكَ خَيْرٌ أَمْ جَنَّةُ ٱلْخُلْدِ ٱلَّتِى وُعِدَ ٱلْمُتَّقُونَ ۚ كَانَتْ لَهُمْ جَزَآءً وَمَصِيرًا

Maana

Sema: Je, haya ni bora au Bustani ya milele, ambayo wameahidiwa wacha Mungu, iwe kwao malipo na marejeo?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Je! Haya ni bora au Pepo ya milele, ambayo wameahidiwa wachamngu, iwe kwao malipo na marejeo? [15]

[15] Ewe Nabii! Waambie makafiri: Je! Marejeo haya waliyo ahidiwa makafiri ni bora au Pepo yenye kudumu neema zake, na ambayo wameahidiwa Waumini, wachamngu, kuwa itakuwa yao kama ndio malipo na marejeo ya kwendea baada ya kufufuliwa na kuhisabiwa?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema uwaambie, ewe Mtume, «Je, Moto huu mliosifiwa ndio bora au ni Pepo ya neema za milele walioahidiwa wenye kuiogopa adhabu ya Allah Mtukufu, ambayo itakuwa yao ikiwa ni malipo ya matendo yao na ni mahali watakapoishia huko Akhera?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net