Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 9

An-Noor 24:9

النور

وَٱلْخَـٰمِسَةَ أَنَّ غَضَبَ ٱللَّهِ عَلَيْهَآ إِن كَانَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Maana

Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, kama mumewe yu miongoni mwa wanaosema ukweli.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mara ya tano ya kwamba ghadhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama mumewe yu miongoni mwa wanao sema kweli. [9]

[9] Na ataje katika mara ya tano kuwa yeye mwanamke anastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu imshukie ikiwa mumewe ni mwenye kusema kweli katika tuhuma yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na aongeze katika ushahidi wake wa mara ya tano kwa kujiapiza kuwa anapaswa kushukiwa na hasira za Allah Mtukufu iwapo mumewe ni mkweli katika madai yake kuwa yeye amezini. Na katika hali hii watatenganishwa baina ya wao wawili.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net