An-Noor 24:10
النوروَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ وَأَنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٌ حَكِيمٌ
Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpokeaji toba na Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpokeaji toba. [10]
[10] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hakukufanyieni fadhila na akakurehemuni, na kuwa Yeye ni Mwingi wa kukubali toba za waja wake, na Mwenye hikima katika vitendo vyake vyote, asingeli kufanyieni sharia za hukumu hizi, na angeli fanya haraka kukuadhibuni duniani kwa maasia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau kama si wema wa Allah Mtukufu juu yenu na rehema Zake kwenu, enyi Waumini, kwa mapitisho haya ya kisheria kwa waume na wake, na kwamba Allah Mtukufu ni Mwenye kuitikia toba kwa aliyetubia miongoni mwa waja wake ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake na maongozi Yake, basi yangempata mmoja wa wale wawili wanaolaaniana yale aliyojiapiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net