An-Noor 24:11
النورإِنَّ ٱلَّذِينَ جَآءُو بِٱلْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ لِكُلِّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُم مَّا ٱكْتَسَبَ مِنَ ٱلْإِثْمِ ۚ وَٱلَّذِى تَوَلَّىٰ كِبْرَهُۥ مِنْهُمْ لَهُۥ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Hakika wale walioleta uongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio leta uwongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyo yachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa. [11]
[11] Hakika hao walio zua uwongo ulio potoka na kila uwongofu kumzulia Aisha, mke wa Nabii s.a.w. walipo mtangazia uzushi, ni kikundi wanao ishi pamoja nanyi. Msidhani kituko hichi ni shari kwenu, bali ndiyo kheri yenu; kwa sababu kimewapambanua baina ya wanaafiki na Waumini wa kweli. Na ukadhihiri ukarimu wa walio wema na wenye kuingiwa na uchungu. Na kila mtu katika hawa walio tuhumu watapata malipo yao kwa mujibu wa kadri alivyo shiriki katika uzushi huu. Na mkuu wa kikundi hichi ndiye ataye pata adhabu kubwa kwa ukubwa wa makosa yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika, wale waliokuja na urongo mbaya kabisa, nao ni kumsingizia Mama wa Waumini ‛Ăishah, radhi za Allah Mtukufu zimshukie, kuwa amefanya kitendo kichafu, ni kikundi cha watu wanaohusiana na nyinyi, enyi kongamano la Waislamu. Msidhanie maneno yao ni shari kwenu, ilivyo ni kuwa maneno yao ni kheri kwenu, kwa kuwa maneno hayo yalisababisha kutakaswa Mama wa Waumini na uchafu, kusafika kwake na kuukuza utajo wake, kuzipandisha daraja, kuyafuta maovu na kuwasafisha Waumini. Kila mmoja aliyeuzungumza urongo huo atapata malipo ya kitendo chake cha dhambi. Na yule aliyebeba jukumu kubwa zaidi katika uzushi huo, naye ni ‛Abdullah bin Ubayy bin Salûl, kiongozi wa wanafiki, Allah Mtukufu Amlaani, atakuwa na adhabu kubwa huko Akhera, nayo ni kukaa milele motoni».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net