An-Noor 24:12
النورلَّوْلَآ إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ ٱلْمُؤْمِنُونَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا۟ هَـٰذَآ إِفْكٌ مُّبِينٌ
Kwa nini mlipoisikia habari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhahiri?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa nini mlipo sikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri? [12]
[12] Ilikuwa inavyo takikana kwa Imani ni kuwa wakati wa kusikia huu uzushi, ni Waumini wanaume na wanawake wajidhanie nafsi zao kheri ya usafi na unadhifu, na waseme kwa kupinga: Huu ni uwongo ulio wazi umezuliwa, kwa kuwa haya yamemkhusu bora ya Mitume na bora ya wanawake walio wa kweli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Si ingekua bora kwa Waumini wanaume na wanawake wadhaniane kheri wao kwa wao pindi waliposikia uzushi huo, kuwa yale waliyosingiziwa hawanayo, na waseme, «Huu ni urongo ulio wazi» juu ya ‘Aisha, radhi za Allah Mtukufu zimfikie.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net