Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 8

An-Noor 24:8

النور

وَيَدْرَؤُا۟ عَنْهَا ٱلْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَـٰدَٰتٍۭ بِٱللَّهِ ۙ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ

Maana

Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu, ya kwamba huyu mume ni miongoni mwa waongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba huyu mume ni miongoni mwa waongo. [8]

[8] Baada ya haya mwanamke akinyamaza kimya itampasa kupata adhabu ya uzinzi. Ili kujikinga na adhabu yampasa ashuhudie kwa Mwenyezi Mungu mara nne kwamba mumewe ni mwongo kumtuhumu yeye kwa uzinzi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa ushahidi wake huu, itapasa kwa yule mke aliyetuhumiwa kutiwa adabu ya uzinifu, nayo ni kupigwa mawe mpaka kufa. Na haitamuepukia adabu hii mpaka atoe ushahidi wa kupinga ule ushahidi wa mumewe, mara nne kwa jina la Allah Mtukufu kwamba mumewe ni mrongo katika madai yake kuwa yeye amezini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net