Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 64

An-Noor 24:64

النور

أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ قَدْ يَعْلَمُ مَآ أَنتُمْ عَلَيْهِ وَيَوْمَ يُرْجَعُونَ إِلَيْهِ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌۢ

Maana

Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakika Yeye anajua mliyo nayo. Na siku watakaporudishwa kwake atawaeleza waliyoyafanya. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na ardhini. Hakika Yeye anajua mlio nayo. Na siku mtapo rudishwa kwake atawaeleza waliyo yafanya. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. [64]

[64] Zindukaneni enyi watu! Mjue kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kumiliki mbingu na ardhi, na viliomo ndani yao. Anayajua mlio nayo, ukafiri wenu na Uislamu wenu, na uasi wenu, na ut'iifu wenu. Basi msiende kinyume na amri yake. Na Yeye atawapa khabari watu, watapo rejea kwake Siku ya Kiyama, kwa yote waliyo yatenda duniani, na atawalipa kwayo. Kwani Yeye amekizunguka kila kitu kwa ujuzi wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Jueni mtanabahi kwamba ni vya Allah Mtukufu vilivyoko mbinguni na ardhini, kwa kuviumba, kuvimiliki, kuvifanya vimdhalilikie. Ujuzi Wake umevizunguka vyote ambavyo muko navyo. Na Siku ya Akhera, ambayo waja watarejea Kwake, Atawapa habari ya matendo yao, na Atawalipa kwayo. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa kila kitu, hayajifichi Kwake matendo yao na hali zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net