An-Noor 24:63
النورلَّا تَجْعَلُوا۟ دُعَآءَ ٱلرَّسُولِ بَيْنَكُمْ كَدُعَآءِ بَعْضِكُم بَعْضًا ۚ قَدْ يَعْلَمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ يَتَسَلَّلُونَ مِنكُمْ لِوَاذًا ۚ فَلْيَحْذَرِ ٱلَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِۦٓ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanaoondoka kwa kujificha. Basi na watahadhari wanaohalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu. [63]
[63] Fanyeni hima kuhishimu wito wa Mtume kukuiteni kukusanyika kwa mambo muhimu. Na muitikieni huo wito wake, wala msifanye wito huo kama mnavyo itana nyinyi kwa nyinyi, kuwa inafaa kupuuza na kuondoka mpendavyo. Wala msiondoke ila baada ya kutaka ruhusa na mkakubaliwa, na tena iwe katika mipaka ya ufinyo kabisa, na dharura za shida. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu anawajua wanao ondoka bila ya idhini wakijificha ficha kati ya watu ili ati Mtume asiwaone. Na watahadhari wanao kwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu asije Subhanahu akawapatiliza kwa uasi wao wakapata mateso makali duniani kama ukame na mitetemeko, au akawapa adhabu yenye wingi wa uchungu aliyo waandalia Akhera, nayo ni ya Motoni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Msiseme, enyi Waumini, mnapomuita Mtume wa Allah Mtukufu, «Ewe Muhammad!» wala «Ewe Muhammad bin Abdillāh!» kama wanavyosema hivyo baadhi yenu kuwaambia wengine. Lakini mtukuzeni na mseme, «Ewe Nabii wa Allah Mtukufu! Ewe Mtume wa Allah Mtukufu!» Kwa kweli Allah Mtukufu Anawajua wale wanaoondoka kutoka kwenye kikao cha Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa siri, bila ya ruhusa yake, wakisaidiana kujificha. Basi na wajihadhari wanaoenda kinyume na amri Yake wasije wakashukiwa na janga na shari au adhabu yenye uchungu iumizayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net