An-Noor 24:62
النورإِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَإِذَا كَانُوا۟ مَعَهُۥ عَلَىٰٓ أَمْرٍ جَامِعٍ لَّمْ يَذْهَبُوا۟ حَتَّىٰ يَسْتَـْٔذِنُوهُ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَسْتَـْٔذِنُونَكَ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۚ فَإِذَا ٱسْتَـْٔذَنُوكَ لِبَعْضِ شَأْنِهِمْ فَأْذَن لِّمَن شِئْتَ مِنْهُمْ وَٱسْتَغْفِرْ لَهُمُ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Hakika Waumini wa kweli ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na wanapokuwa pamoja naye kwa jambo la kuwakhusu wote hawaondoki mpaka wamtake ruhusa. Kwa hakika wale wanaokuomba ruhusa, hao ndio wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na wakikuomba ruhusa kwa baadhi ya kazi zao, mruhusu umtakaye miongoni mwao, uwaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Waumini wa kweli ni walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na wanapo kuwa pamoja naye kwa jambo la kuwakhusu wote hawaondoki mpaka wamtake ruhusa. Kwa hakika wale wanao kuomba ruhusa, hao ndio wanao muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na wakikuomba ruhusa kwa baadhi ya kazi zao, mruhusu umtakaye miongoni mwao, uwaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemmu. [62]
[62] Hakika Waumini wenye kusadiki ni wale ambao wamemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wala hawamwachi Mtume peke yake katika jambo muhimu linalo hitajia wajumuike pamoja kwa ajili yake, kama mfano wa Jihadi. Ila baada ya kumtaka ruhusa ya kuondoka na wakakubaliwa, hakika wanao kukadiri wewe, ewe Nabii, kama unavyo stahiki, na wanatambua umuhimu wa huo mkusanyiko hawaondoki ila baada ya wewe kukubali. Hao ndio wenye kusadiki katika Imani yao kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi wakikutaka ruhusa hawa kwenda kufanya baadhi ya maslaha yao mpe ruhusa umtakaye katika wao, pindi ukimwona kuwa ana haja kweli ya kuondoka, na si dharura kwa mkutano kuwapo yeye. Juu ya hivyo waombee maghfira kwa Mwenyezi Mungu kwa kuondoka kwao, ambako kwa hakika hakuelekei kabisa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa maghfira na rehema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika Waumini kikwelikweli ni wale ambao Wamemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakazifanyia kazi sheria Zake, na wakiwa wapo pamoja na Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), katika jambo ambalo amewakusanya kwalo la maslahi ya Waislamu, hawaondoki mpaka wamuombe ruhusa. Kwa hakika wale wanaokuomba ruhusa, ewe Nabii, ndio wanaomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake kikweli. Basi wakikuomba ruhusa kwa baadhi ya haja zao, mruhusu unayemtaka miongoni mwa wale waliokuomba ruhusa kuondoka kwa udhuru, na uwaombee msamaha kwa Allah Mtukufu, kwani Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za waja Wake wenye kutubia, ni mwingi wa huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net